
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliodhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) akimlaki Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha kufungua warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifafanua jambo kuhusu warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na ESRF kwa mgeni rasmi (aliyeipa mgongo kamera) na meza kuu kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano

Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliohudhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya uwasilishaji wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya iliyofanyika jijini Arusha katika hoteli ya Ngurdoto.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)

Naibu Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akiwasilisha mada ya Mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea: kuangalia zaidi ukaji wa uchumi wakati wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa kwa Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 na Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa iliyofanyika katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
